AfricaTube

IMERATIBIWA NA KITUO CHA SANAA CHA WAZA

Kila baada ya miezi sita, Kituo cha Sanaa cha Waza kilichopo Lubumbashi (Nchi ya Kidemokrasia ya Kongo) huwasilisha machaguo mapya katika maonesho haya ya kazi za sanaa kutoka katika Jukwaa la Mtandaoni la Kiafrika. Matokeo yake ni uwepo wa fursa ya kupiga mbizi kimawazo katika mtandao huo, hasa ukichagizwa na mipango ya vijana waishio Kongo, na mahali pengine katika bara au waishio ughaibuni. Kazi zao zinavuka mipaka ya nchi na vikwazo vyote viwekwavyo.

< World Kiswahili Day