Afropea

Watu kutoka nchi nyingi za Kiafrika za kusini mwa Jangwa la Sahara wamefika Ubelgiji baada ya Ukoloni. Jamii ndogo ya Wakongomani iliishi hapa kabla au muda mfupi baada ya uhuru mwaka 1960, lakini kundi kubwa limewasili Ubelgiji baada ya mwaka 2000. Kwa sasa, nchi za Kiafrika za Kusini mwa Sahara zinawakilisha asilimia 2 ya watu wa Ubelgiji; ambao asilimia 40 kati yao ni kutoka Kongo. Tafiti zinaonesha kuwa watu hawa wanakumbana na ubaguzi wa rangi wa hali ya juu. Japokuwa hawapewi fursa kubwa katika majadiliano ya kijamii, wana mchango mkubwa ndani ya umma wa Ubelgiji.

Hiki chumba hutumika kama maonesho, sehemu ya kukutana na mahali pa kuandalia makala mbalimbali. Chumba hiki kiliandaliwa kwa ushirikiano mkubwa na Waafrika wa kusini mwa Sahara. Wageni wanakaribishwa kupendekeza maboresho, kuleta hati, picha na shuhuda mbalimbali ili tuongeze ufahamu wetu. Unaweza kutuma hivi vitu kupitia afropea@africamuseum.be

< World Kiswahili Day