Historia ya Ukoloni
na Uhuru

Kwa kutumia muktadha wa historia ndefu ya Kongo, Rwanda na Burundi, kipindi cha ukoloni kilikuwa kifupi. Lakini, kipindi hicho ndio kimeamua kwa kiwango kikubwa mageuzi mbalimbali ya jamii baada ya ukoloni katika nchi hizi tatu na kutengeneza taswira yao nchini Ubelgiji.

Kimsingi, kwa sasa, wanahistoria wanakubaliana kuujenga kwa upya mtazamo na taswira ya wakati wa ukoloni, lakini katika muktadha wa majadiliano ya umma, ukoloni unabakia kuwa kipindi kilichokuwa na mambo mengi yenye utata. Mikusanyiko iliyopo katika Makumbusho ya Kasri ya Afrika ya Kati (MKAK/RMCA) imetengenezwa na Wazungu. Hii inasababisha changamoto kubwa kuisimulia historia hiyo kwa mtazamo wa kiafrika. MKAK/RMCA inataka kuchochea hamu katika kipindi hiki, na hasa kuamsha midahalo ya mara kwa mara kuhusu hili.

< World Kiswahili Day