Chumba cha Mamba

Makumbusho haya yameamua kwa kusudi kabisa kukigandisha chumba hiki. Kinaonesha namna asili ya Kikongo ilivyokusanywa, kutunzwa, kutafsiriwa na kuoneshwa miaka ya 1920.

Michoro ya mandhari na picha za zamani zisizo na rangi, zinaonesha Afrika ngeni na yenye mahaba. Picha hizo zinaonesha maisha ya kila siku ya Wakongomani katika mandhari safi ambayo bado haijaguswa na ukoloni. Kwa muda mrefu, picha kama hizo nzuri zimewabadili mtazamo wa awali waliokuwa nao wageni wa makumbusho haya juu ya Kongo.

< World Kiswahili Day