Taswira

RMCA ina mkusanyiko mkubwa wa picha na filamu za wakati wa ukoloni ambazo zilitengenezwa na Wazungu na zinaonesha kwa kiasi kikubwa mtazamo wao. Kupitia taswira hiyo, waliamua kwa kiasi kikubwa mtazamo wa watu juu ya Afrika ya Kati na pia wa Waafrika mpaka baada ya ukoloni na hata mpaka sasa. Kupitia mtazamo huo, walitoa ushawishi kwa wapiga picha na watengeneza filamu kuwa na mtazamo huo pia.

Eneo hili linatoa fursa ya nyenzo mbalimbali za kukusaidia kuelewa zaidi picha na filamu.
Maoni, picha, vitabu na sanaa za kiafrika zinawaalika wageni kutafakari kwa muono mpya namna ya kuiwasilisha taswira ya Afrika ya Kati.

< World Kiswahili Day