Chumba cha Utangulizi

MAKUMBUSHO MWENDONI

Makumbusho ya Kasri ya Afrika ya Kati ni kituo cha kisayansi cha Afrika na kiungo muhimu cha utamaduni na vizazi.

Makumbusho haya yalitokana na maonesho ya dunia wakati wa ukoloni yaliyofanyika mwaka 1897 kwa uanzilishi wa Mfalme Leopold wa pili ambaye alitumia Makumbusho haya kama nyenzo ya kuwasilisha propaganda za kuipamba miradi yake ya kikoloni itazamwe kuwa ni chanya. Yalianzishwa kama “Musée du Congo” yakitumia mapato kutoka Taifa Huru la Kongo. Mapato hayo yalitokana na uvunaji wa mpira ambao ulitawaliwa na ukatili mkubwa na kazi ngumu za kulazimishwa.

Makumbusho yana utaalamu mkubwa katika sayansi asilia ya kimaisha na ina makusanyo mbalimbali ya aina tofauti tofauti. Makumbusho haya yanafanya kazi kwa ushirika na Makumbusho ya Kiafrika, taasisi za utafiti, na wataalamu mbalimbali. Kila mwaka, Makumbusho huchangia katika mafunzo ya wanasayansi na wafanyakazi wa umma watokao bara la Afrika zaidi ya 100.

RMCA/MKAK ina mchango muhimu katika usambazaji wa uelewa kuhusu Afrika na ni mdau muhimu katika miradi mbalimbali ya kitafiti ya kimataifa.

< World Kiswahili Day