Mandhari na
Viumbe hai

Ndani ya Afrika, kuna majangwa makubwa, nyika pana, milima yenye barafu, na mojawapo ya misitu mikubwa ya mvua duniani. Kila sehemu, kuna mimea na wanyama waliokubaliana na kukabiliana na hali ya sehemu husika, hasa katika maeneo magumu.

Lakini, upekee huu wa viumbe hai uko katika shinikizo kubwa.

Je, kuna mwingiliano gani kati ya watu, wanyama, mimea na hali ya hewa? Ni kwa namna gani wanadamu wameathiri asili, na nini kitatokea hapo mbele? Tunavyozidi kupata ujuzi na maarifa zaidi, ndivyo tunavyozidi kupata majibu kwa maswali haya muhimu.

< World Kiswahili Day