Historia ndefu

Kimsingi, Afrika ya Kati ina historia ndefu, pana na yenye utajiri mkubwa; ila haijulikani sana.

Ili kuweza kusimbua tamaduni zingine mbalimbali, pamoja na mifumo ya kisiasa na kiuchumi, unatakiwa kuwa na fungu sahihi la funguo. Unatakiwa kufahamu, mathalani, chuma kilikuwa ni alama ya nguvu, pia shaba na sio dhahabu; ndio yalikuwa madini ya thamani kiuchaguzi. Chumba hiki kinakupatia funguo kadhaa wa kadhaa. Pia kinakuonesha namna ambavyo zamani na sasa zinaingiliana, namna ambavyo nidhamu za kisayansi zinafanya kazi pamoja kutengeneza upya Historia ya Afrika ya Kati - na namna ambavyo kuna fursa kubwa ya kugundua mambo mengi katika historia hiyo.

< World Kiswahili Day