Kitendawili cha
Ki-rasilimali

Uchumi wa dunia unategemezwa na rasilimali asilia. Afrika ya Kati na hususani Kongo zina rasilimali asilia nyingi sana.

Ukanda huu unabakia kuwa kivutio cha kiuchumi japokuwa una machafuko ya kisiasa ambayo yanachochewa kwa kiasi kikubwa na mataifa yenye nguvu katika dunia ya utandawazi.

Kitendawili cha Utoshelevu: Afrika ya kati pamoja na kuwa na utajiri mkubwa, bado watu wake ni maskini sana. Iwapo utawala bora unaojikita katika maendeleo endelevu ungetumika, ungesaidia ustawi wa ukanda huu. Sambamba na hilo, uwepo wa idadi kubwa ya watu tena wenye desturi mbalimbali katika Afrika ya Kati ungeistawisha zaidi kimaendeleo.

< World Kiswahili Day