7 July 2022 - World Kiswahili Day

Jumba la Makumbusho la Afrika laadhimisha Siku ya Kiswahili duniani!
""

Ukikaa ukitulia mengi utayasikia

 

Mwaka uliopita UNESCO (Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni) liliitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani. Kiswahili ni lugha ya kwanza kusherehekewa hivyo ikitarajiwa kuwa haitakuwa lugha ya mwisho. Pamoja na ubalozi wa Tanzania jumba la makumbusho linaadhimisha shani hii.

Kiswahili kilitokana awali kwenye pwani za Afrika ya Mashariki kikakulia kuwa lugha inayosemwa kupita zote Afrika ya Mashariki. Kina wasemaji milioni 80, siyo Tanzania na Kenia tu, ambamo Kiswahili ni lugha rasmi na ya kitaifa, lakini tena katika nchi nyinginezo za Afrika ya Mashariki kama vile Visiwa vya Ngazija, sehemu za mashariki za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi na Uganda.

Tarehe 7 mwezi wa Julai jumba la makumbusho pamoja na ubalozi wa Tanzania wanasherehekea siku ya kwanza ya Kiswahili duniani. Waongozi wasimamishi watakueleza umuhimu wa Kiswahili katika onyesho la kudumu. Tena utaweza kufuata somo la kwanza la Kiswahili kutoka kwa walimu wenye uzoefu au utapashwa madokezo kwa kuwapokeza watoto Kiswahili. Mwanaisimu atazungumzia asili ya Kiswahili na watoto watajitosa katika maajabu ya methali au watajifunza kuvaa kanga na haswa kupeana ujumbe nazo. Njoo tu, utayasikia mengi!

 

 


 

AfricaMuseum
Leuvensesteenweg 13
3080 Tervuren

Info

More information coming soon.